Leo nitaanza kwa kuelezea kwa mhutasari namna ambavyo afya ya udongo (Soil fertility) inaweza kutunzwa na kuendelezwa ili kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali. Afya ya udongo inaathiriwa sana na aina ya virutubisho/Madini yaliyomo na hii ndiyo kusema aina ya mbolea itumiwayo katika kurutubisha mazao mbalimbali shambani inamchango wa moja kwa moja katika afya ya udongo.
Mbolea ni nini?
Mbolea ni kirutubisho cha udongo chenye uwiano sahihi wa virutubisho vyote vinavyohitajika kwa ukuaji wa mmea hasa Nitrojeni, Fosforasi na potasiam. Pia aina nyingine za virutubisho zinahitajika katika kiwango kidogo ingawa zina umhimu wake katika hatua mbalimbali za ukuaji wa mimea. Kuna aina mbili za mbolea ambazo ni Mbolea za viwandani na mbolea za asili.
Sifa za mbolea za viwandani
(i)Zinaachia virutubisho kiurahisi
(ii)Ni rahisi kupotea katika mtindo wa gesi au kubanwa na madini mengine yaliyopo kwenye udongo
(iii)Uwiano wa virutubisho vyake unajulikana.
(iv)Ikitumiwa kwa muda mrefu inaweza kuleta madhara kwenye afya ya udongo
(v)Inayumika kwa kiasi kidogo
Sifa za mbolea za asili
(i)Zinaachia virutubisho polepole
(ii)Zinasaidia kutunza unyevunyevu na kurekebisha sura ya udongo
(iii)Hazina madhara kwa wadudu waozeshaji(effective microorganism) na zinaweza kutumiwa kwa muda mrefu
(iv)Haihitaji gharama kubwa kutengeneza
(v) Inahitaji kiasi kikubwa kwa shamba
(Vi)Mkulima yeyote anaweza kutengeneza
Utengenezaji wa Mbolea za asili: Kuna njia kuu tatu za utengenezaji wa mbolea hizi nazo ni uozeshaji kwa kutumia biwi, Uozeshaji kwa kutumia wadudu waozeshaji na njia ya Bokashi. Tutazungumuzia kiundani zaidi katika makala zitakazofuata.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni